Kocha wa Barcelona Enrique kujiuzulu Kocha wa klabu ya Barcelona Luis Enrique ametangaza kwamba atabwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu.

Enrique atakuwa amehudumu kama meneja wa klabu hiyo kwa misimu mitatu.

Aliishindia klabu hiyo kombe la vilabu bingwa na mataji mengine mawili alipojiunga na Barcelona na kuwasaidia kushinda makombe 2 mwaka uliopita.

Lakini licha ya klabu hiyo kuongoa katika jedwali la ligi Barcelona iko katika hatari ya kubanduliwa katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu huu baada ya kufungwa 4-0 na Prais St-Germain.

Enrique amesema kuwa sababu kuu ya yeye kutaka kujiuzulu ni kwamba anahitaji kupumzika.
Sambaza kwenye Google Plus

About HB Mtetezi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment