Ngassa awafungukia Simba

MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Mrisho Ngasa, amesema "sina maneno" ya kuwaambia Simba badala yake wasubiri kuona vitendo vyake uwanjani.

Ngasa alisema pia mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizobakia ni ngumu na lolote linaweza kutokea huku akiainisha kuwa mbio za kusaka ubingwa wa ligi hiyo ziko wazi.

Simba inatarajia kuikaribisha Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ngasa, alisema amefanya mazoezi vizuri na anaamini mechi hiyo itasaidia kuendeleza heshima yake kwenye Uwanja wa Taifa.

"Najua ni mechi ngumu, tumepoteza mechi mbili nyumbani hivi karibuni, tunahitaji kupambana ili kurejea kwenye ushindani, Simba tunaifahamu na tunaiheshimu," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Kagera Sugar, Yanga, Azam FC, Simba na Free State Stars ya Afrika Kusini.

Mshambuliaji huyo aliongeza: "Kuna wanaowania ubingwa wa msimu huu, watacheza kwa mipango yao, kuna wanaohitaji kubaki kwenye ligi wasishuke daraja nao hao lazima wakomae, na sisi tutaingia uwanjani ili kusaka pointi tatu kwa sababu tunaamini mbio za ubingwa ziko wazi."

Aliongeza kuwa mechi zote za ligi zilizobakia ni ngumu kwa sababu kila timu inashuka uwanjani ikiwa na malengo tofauti.
Sambaza kwenye Google Plus

About HB Mtetezi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment