Operesheni ya viroba inaendelea- Majaliwa


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema operesheni kuhusu pombe za viroba inaendelea katika mikoa mbalimbali baada ya kupigwa marufuku Machi Mosi.

Majaliwa amesema hayo katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha kwanza tangu Serikali kuhamia mjini hapa.

 Amesema katika operesheni hiyo wamegundua mambo mengine ikiwamo uwapo wa kampuni zilizokuwa hazilipi kodi.

Kuhusu kikao hicho cha mawaziri, Majaliwa amesema wizara zitatoa takwimu za watumishi waliohamia, idadi ya watumishi wote, wamepanga awamu ngapi za kuhamia Dodoma kati sita zilizopangwa na Serikali.

“Ningependa kujua ofisi zenu ziko wapi kwa sababu baadaye nitafanya ziara kuona shughuli zinazoendelea na kazi ya utoaji wa huduma ili kujiridhisha  na Watanzania kwamba azma yetu ya kuhamia Dodoma imekamilika,”amesema.
Sambaza kwenye Google Plus

About HB Mtetezi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment