Singapore kutangaza utalii wa Zanzibar


Balozi wa Singapore nchini, Tan Puay Hiang ameahidi kuitangaza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  katika sekta ya utalii ili kuimarisha ushirikiano.

Hiang ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.

Amesema nchi hiyo itazidisha uhusiano katika sekta za usafirishaji, uwekezaji, afya na biashara pamoja na kubadilishana utaalamu.

Hiang  amesema wameona umuhimu wa kuwapo  ushirikiano katika kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa viongozi.

Dk Shein amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Singapore na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwamo Zanzibar kwa kipindi kirefu.

Wakati huohuo, Dk Shein amefanya mazungumzo na mabalozi wa Tanzania walioteuliwa na kuapishwa hivi karibuni na Rais John Magufuli.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu mjini Zanzibar. Miongoni mwa mabalozi hao ni Pindi Chana anayekwenda nchini Kenya, Abdalla Kilima (Oman), Joseph Sokoine (Ubelgiji), Silima Kombo Haji (Sudan),  Fatma Rajab ( Qatar), Batilda Masuka (Korea) na Grace Mgovano (Uganda).

 Dk Shein amewapongeza kupata uteuzi huo kutokana na sifa walizonazo katika utendaji wao.
Sambaza kwenye Google Plus

About HB Mtetezi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 Maoni:

Post a Comment